Hadiyth “Sema ´Namuamini Allaah`, kisha… “

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

21- Abu ‘Amr, vilevile imesemekana kuwa [anaitwa] Abu ‘Amrah Sufyaan bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza: “Nilisema: “Ee Mtume wa Allaah! Nieleze kitu juu ya Uislamu ambacho sintomuuliza mtu yeyote zaidi yako.” Akamwambia: “Sema: “Namuamini Allaah”, kisha uwe na msimamo.”

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Sema “Namuamini Allaah.”

Kama tulivyotangulia kusema ya kwamba imani ni: kauli, matedno na I´tiqaad. Akisema:

“Namuamini Allaah.”

Bi maana atakuwa ameamini I´tiqaad sahihi na ametenda matendo sahihi na mema yaliyoafikiana na Sunnah na akawa ni mwenye kumtakasia nia Allaah (Jalla wa ´Alaa). Vilevile amezungumza na kutamka Anayoyapenda Allaah (Jalla wa ´Alaa).

Kwa hivyo, maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Namuamini Allaah.”

Kunaingia ndani yake maneno, matendo na I´tiqaad. Ndani ya wasia huu kumeingia dini yote. Kwa sababu alisema:

“Nieleze kitu juu ya Uislamu ambacho sintomuuliza yeyote zaidi yako.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Sintomuuliza yeyote baada yako.”

Akamwambia:

“Sema: “Namuamini Allaah.”

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 305
  • Imechapishwa: 14/05/2020