Hadiyth “Ishi duniani kama vile mgeni au mpita njia”

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

40- Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimshika bega na akasema:

“Ishi duniani kama vile mgeni au mpita njia.”

Huu ni wasia mkubwa lau watu wangeliutia akilini. Hakika ya mwanaadamu maisha yake yalianzia Peponi na akateremshwa katika ardhi hii ili kupewa mtihani. Katika dunia hii ni kama mgeni au mpita njia. Haya ni matembezi ya kigeni. Mahala khaswa pa Aadam na wale wote watakaomfuata katika imani, taqwa, kumpwekesha Allaah (Jalla wa ´Alaa) na kumtakasia Yeye dini, ni Peponi. Aadam alitolewa Peponi kwa majaribio na malipo kutokana na aliyoyafanya. Hivyo mja muislmu, ukizingatia hili vizuri basi utaona kuwa makazi yako ya kikweli ni Peponi na si duniani. Dunia ni nyumba ya majaribio. Yeye ni kama mgeni au mpita njia kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 520
  • Imechapishwa: 10/05/2020