Hadiyth dhaifu kwa mujibu wa Ahmad

Swali: Tunawasikia baadhi ya maimamu wanasema kuwa endapo masuala fulani hayawezi kuthibitishwa kwa Hadiyth Swahiyh basi inaweza kutumiwa Hadiyth dhaifu. Wametoa mfano kwa imamu Ahmad. Kunakusudiwa nini kwa Hadiyth dhaifu hapa?

Jibu: Kwa mujibu wa Ibn Taymiyyah anacholenga Imaam Ahmad ni ile Hadiyth ambayo hii leo inaitwa “nzuri” (حسن). Wakati wa Imaam Ahmad “Hadiyth nzuri” haikuwa ni mtindo ulioenea sana. Wakati huo Hadiyth zilikuwa zimegawanyika sehemu mbili:

1- Swahiyh.

2- Dhaifu.

Wakati inapokuja kutoka kwa Imaam Ahmad ya kwamba ni sawa kutendea kazi Hadiyth dhaifu katika suala fulani ikiwa hakuna nyingine, anamaanisha Hadiyth iliyothibiti kwa daraja ya chini ya kuthibiti, nayo si nyingine ni Hadiyth nzuri. Haya yanatambulika kwa yule mwenye kujishughulisha na elimu hii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (01)
  • Imechapishwa: 16/09/2017