Hadiyth dhaifu kuhusu Sha´baan


Swali: Wanachuoni wanasemaje juu ya elimu ya Hadiyth katika Athar hii:

رجب شهر الله ، وشعبان شهري ، ورمضان شهر أمتي

“Rajab ni mwezi wa Allaah, Sha´baan ni mwezi wa kawaida na Ramadhaan ni mwezi wa Ummah wangu.”?

Ni upi usahihi wa Hadiyth:

اللهم إني أشكو إليك ضعف قوتي ، وقلة حيلتي ، وهواني على الناس

“Ee Allaah! Hakika mimi nakushtakia Wewe udhaifu wa nguvu zangu, uchache wa hila zangu na udhaifu kwa watu… ”?

Jibu: Hadiyth ya kwanza imetungwa. Katika cheni ya wapokezi wake yuko myu anayeitwa Abu Bakr bin al-Hasan an-Naqqaash. Ni mwenye kutuhumiwa. al-Quswaa-iy hajulikani. Mtunzi wa kitabu “al-Lu´lu´ fiyl-Mawdhwu´aat” amemtaja.

Kuhusu Hadiyth ya pili ni dhaifu kwa upande wa mlolongo wa wapokezi.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=2&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 18/04/2018