Haddaadiyyah wamehuisha Bid´ah za zamani

Swali: Je, Haddaadiyyah wamevumbua kanuni inayooenda kinyume na Ahl-us-Sunnah?

Jibu: Ndio. Haddaadiyyah wamevumbua kanuni ambayo wamehuisha Bid´ah za zamani, nazo ni Bid´ah za Takfiyr. Haddaadiyyah wana misingi mitatu ya khatari:

1- Inapokuja katika Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ hawajali kuwasimamishia hoja na kuondosha utata. Kila anayetumbukia katika Bid´ah wanamtoa katika Sunnah, Uislamu na Dini. Hali imekuwa mbaya kiasi cha kwamba wamefikia baadhi yao kusema kuwa vitabu “Fath-ul-Baariy” na ufafanuzi wa an-Nawawiy wa “as-Swahiyh” ya Muslim viunguzwe. Mpaka baadhi yao wamenambia kuwa hata “Majmuu´-ul-Fataawaa” ya Ibn Taymiyyah inastahiki kuunguzwa. Watu wameenda kinyume na Ahl-us-Sunnah katika kanuni hii. Wao hawana kitu kinachoitwa kumsimamishia hoja mtu mwenye kutumbukia kwenye kosa au kwenye Bid´ah.

2- Hawatofautishi kati ya matangamano kwa mwanachuoni anayefanya kosa na matangamano ya Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ kutokana na Bid´ah na matamanio yao. Wanatangamana na Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ na Ahl-us-Sunnah sawa sawa. Ahl-us-Sunnah wanasema kuwa wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah hawakukingwa na kukosea. Mwanachuoni mkubwa wa Ahl-us-Sunnah anaweza kutumbukia kwenye kosa. Katika hali hii Sunnah ya mtu ni yenye kukubaliwa na kosa lake ni lenye kurudishwa. Hakukingwa na kukosea. Tunasema kuwa hakuna yeyote aliyekingwa na kukosea. Ni kosa, lakini hata hivyo ni kosa la mwanachuoni. Kupitia mfumo wake na madhehebu yake tunajua kuwa anaadhimisha Sunnah na anafuata Salaf na mapokezi, lakini ametumbukia kwenye kosa katika jambo fulani. Kwa sababu tu ni mwenye kujinasibisha na Sunnah na Salafiyyah haina maana ya kwamba hawezi kufanya kosa. Ni nani alosema hivi? Ni nani katika Salaf alosema hivi? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila binaadamu ni mwenye kukosea na wabora katika wakoseaji ni wale wenye kutubia.”

Mwanachuoni katika Ahl-us-Sunnah akikosea, bado ataheshimiwa na kutambua hadhi yake. Upupiaji wake na uadhimishaji na ufuataji wake wa Sunnah utakubaliwa na wakati huo huo kosa lake litarudishwa. Atataamiliwa kwa njia maalum na sio kama Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´. Hii haina maana ya kupima kwa mizani au vipimo viwili tofauti. Haya tumefunzwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Namna hii ndivyo walivyokuwa Salaf wakati mwanachuoni au kijana katika Ahl-us-Sunnah anapotumbukia katika kosa. Ni nani aliyesema kuwa vijana wa Ahl-us-Sunnah na Salafiyyah hawakosei? Wanakosea kama wengine. Lakini ikiwa tunajua kuwa kuna kijana anayefuata Sunnah na kuzitilia uzito mkubwa na akatumbukia kwenye kosa, kosa hilo sio kama la mtu mwenye kufuata matamanio na anafuata mfumo wa Ahl-ul-Bid´ah na anatafuta makosa ya Ahl-us-Sunnah.

3- Hawawaheshimu wanachuoni. Wao huwalenga siku zote wanachuoni Salafiyyah na si wengine. Wanawalenga wao, wanawasema vibaya, wanaandika kuhusu wao na kuwanyanyasa.

Nukta hizi tatu zinapatikana kwa Haddaadiyyah. Hizi ndio nukta khatari zaidi walonazo. Mpaka wanawasemea uongo wanachuoni na kusema vibaya na kuwanasibisha kwa Bid´ah. Kubwa walonalo ni kumtuhumu mtu kuwa ni Murji-ah na kwamba ana Irjaa´.

Haddaadiyyah wana nukta hizi tatu za khatari. Ni lazima wakumbushwe nazo, waziache na kuwafuata Salaf.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin ´Umar Baazmuul
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=146687
  • Imechapishwa: 11/04/2015