Swali: Je, tuwatahadharishe wale wanaomkufurisha Ibn Hjar na an-Nawawiy (Rahimahumaa Allaah)?

Jibu: Wanasihi waache jambo hilo. Hawa ni wajinga. Ibn Hjar na an-Nawawiy ni maimamu; ni maimamu wa waislamu na Muhaddithuun. Wana fadhila. Ikiwa walikosea wakati wa kusimulia baadhi ya nukuu, basi itambulike kuwa mnukuaji hana kosa. Inasemekana kuwa yule mwenye kunukuu ukafiri sio kafiri. Katika maelezo yao wananakili yanayosemwa na wengine. Wasichukuliwe kwa hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (62) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd14-07-%201438.mp3
  • Imechapishwa: 22/07/2017