Kuhusu kuwanasihi Ahl-ul-Bid´ah na kukaa nao kwa ajili ya kuwanasihi, mimi siendi majumbani mwao wala katika vikao vyao kufanya hivo. Pindi mmoja wao anakuja nyumbani kwangu namnasihi na kumbainishia haki. Hili si kosa. Pindi wanafiki walipokuwa wakihudhuria vikao vya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwanasihi na kuwabainishia Uislamu na haki.

Ahl-ul-Bid´ah walikuwa wakija kwenye vikao vya Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) anawanasihi na kuwabainishia haki. Hali kadhalika nafikiri kuwa Muftiy na kamati ya Kibaar-ul-´Ulamaa´ wanafanya hivo pindi Ahl-ul-Bid´ah wanapowajia katika Muslim World League na vikao vyao. Simjui mwanachuoni yeyote aliyenambia kuwa mimi nakaa na Ahl-ul-Bid´ah. Wala hakuna yeyote aliyeniraddi kwa hilo. Ni moja katika uongo mwingi wa Fawziy al-Bahrayniy. Huenda hii ndio tabia yake unachanganyika na Ahl-ul-Bid´ah kwa ajili ya kukusanya pesa ili kuzitumia kwa kutumia jina la Uislamu na jina la mwengine.

Kuhusu masuala ya Safar, Salmaan na al-Qarniy, sijui yanahusiana na nini mbali na mizozo iliyopitika kati yangu mimi na wao. Ruduud zangu kwa Salmaan na Safar zinajulikana na Ruduud zangu kwa mwalimu wao Sayyid Qutwub zinajulikana. Mizozo yetu na wao na pamoja na kipote chao inajulikana.

Lakini ziko wapi Ruduud za Haddaadiyyah wa kale na wa sasa juu ya Sayyid Qutwub na watu hawa? Vipi watawaraddi ilihali wao ni wabaya zaidi kuliko wao na wana chuki yenye nguvu dhidi ya Ahl-us-Sunnah na vita vikubwa dhidi yao kuliko wanavyofanya wao?

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 75-76
  • Imechapishwa: 09/10/2016