Haddaadiyyah ndio warithi wa Khawaarij


Fawziy al-Bahrayniy amesema:

“Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy (Rahimahu Allaah) amesema katika “al-Masaa-iyl”[1]: “Khawaarij wanawaita Ahl-us-Sunnah kuwa ni “Murji-ah”. Khawaarij wanasema uongo. Wao ndio Murji-ah kwa sababu wanaona kuwa wao wenyewe tu ndio waumini pasi na wengine ambao wanaona kuwa ni makafiri.” al-Burkaan, uk. 19.

Lau mtu huyu angelikuwa na akili hata kidogo basi asingelitaja nukuu hii inayomfichua yeye na Haddaadiyyah yake. Wao ndio wenye kufuata mapito ya Khawaarij pindi wanapowatuhumu Ahl-us-Sunnah kwa Irjaa´ na wanaandika kwa ajili ya kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah; vitabu vilivyojengwa juu ya uongo na upotoshaji wa maneno ya wanachuoni na Ahl-us-Sunnah.

Haddaadiyyah, warithi wa Khawaarij, wanasema uongo pindi wanapowapiga vita Ahl-us-Sunnah na kuwatuhumu Irjaa´. Wao ndio Murji-ah kwa kuwa wanaonelea wao tu ndio Ahl-us-Sunnah ilihali wanawatuhumu wale Ahl-us-Sunnah wanaopingana nao ya kwamba ni Murji-ah, Khawaarij, Raafidhwah na Baatwiniyyah. Khawaarij wana akili na uadilifu zaidi kuliko Fawziy al-Bahrayniy na genge lake la kimadhambi Haddaadiyyah.

[1] Uk. 366.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 31
  • Imechapishwa: 09/10/2016