Ghafla anataka kwenda msikitini mvua inaanza Kkunyesha       

Swali: Nina ruhusa ya kuswali nyumbani kwangu mvua ikinyesha na nikasikia adhaana ya ´ishaa au ni lazima kuitikia muadhini na kwenda msikitini?

Jibu: Tumesema kuwa ikiwa unapata tabu ya kutoka kwenda msikitini hakuna neno ukaswali nyumbani. Lakini ikiwa uko pamoja na wanaume wengine, sawa wawe ni watoto wako au wanaume wengine, swalini mkusanyiko. Ni sawa wakaswali nyumbani hata kama watakuwa na kipando. Lakini hakuna shaka yoyote lililo bora ni wewe kutoka na kwenda msikitini kuswali na waislamu wenzako. Lakini hata hivyo uko na ruhusa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (05)
  • Imechapishwa: 02/05/2020