Swali: Wakati niliponunua gari kutoka kwa bwana mmoja nilimuuliza kama gari yake ina kasoro yoyote. Jawabu lake lilikuwa kwamba iko katika ukaguzi na hakunibainishia chochote. Je, jawabu lake ni aina fulani ya ulaghai?

Jibu: Ikiwa muuzaji anatambua kuwa gari ina kasoro lakini hata hivyo akaificha, mnunuzi ana haki ya kurudisha. Lakini ikiwa hajui kasoro yoyote ambapo kukabainika kasoro ambayo hakuwa anaijua na haitambuliki kama ilizuka kabla au baada ya ununuzi, basi mnunuzi hana haki yoyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 29/01/2022