Swali: Je, inajuzu kupeleka chakula misikitini wafuturu waliofunga?

Jibu: Hakuna ubaya na Allaah awajaze  kheri. Hii ni ´amali nzuri na njema kufuturisha waliofunga baada ya kuzama kwa jua katika misikiti. Lakini jiepusheni na kuleta vitungu saumu na mfano wake msileta wakati wa futari. Kwa kuwa Mtume (´alayhis-Salaam) kaamrisha aliekula vitu hivi ajitenge na Misikiti yetu. Futari isiwe na vitu hivi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020