Njia hizi zenye nguvu kutoka kwa wapokezi waaminifu zinathibitisha kwamba Hadiyth ni Swahiyh[1]. Haya ndio yanatakiwa kuwa malengo ya utafiti wa Muhaddith.

Kuhusiana na kwamba Hadiyth inapingana na Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy  iliyothibiti kwa al-Bukhaariy na kwa Muslim, hivyo hakuna kugongana kati ya hayo mawili. Kwani Hadiyth inayozungumzia kufunga mlango sio ile Hadiyth inanyozungumzia kufunga penyezo. Kwa sababu nyumba ya ´Aliy bin Abiy Twaalib ilikuwa ndani ya msikiti, ilikuwa jirani na nyumba ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Qaadhwiy Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy amesema katika “Ahkaam-ul-Qur-aan”:

”Ibraahiym bin Hamzah ametuhadithia: Sufyaan bin Hamzah ametuhadithia, kutoka kwa Kathiyr bin Zayd, kutoka kwa al-Muttwalib (bin ´Abdillaah bin Hantwab) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa hamwachi yeyote kupita msikitini wala kukaa baada ya kuwa na Janaabah[2] isipokuwa ´Aliy bin Abiy Twaalib kwa sababu nyumba yake ilikuwa msikitini.”

Hadiyth hii ni Mursal na inatiwa nguvu na Hadiyth ya at-Tirmidhiy kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Aliy:

“Haruhusiwi yeyote zaidi yako wewe na mimi kukanyaga msikiti huu ilihali yuko na janaba.”

Haya yanahusiana na ile milango iliyofungwa.

Ama kuhusu kuziba upenyo/pengo, makusudio ni geti iliokuwa mwanzoni mwa msikiti. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha wakati wa kukata kwake zifungwe penyo zote isipokuwa tu upenyo wa Abu Bakr. Hapa kuna kuashirio juu ya ukhaliyfah wa Abu Bakr kwa sababu yeye ndiye angelikuwa ni mwenye kuhitajia msikiti zaidi kuliko mwengine yeyote.

Kutokana na uoanishaji huu, tunapata kuona kuwa hakuna mgongano wowote kati ya hizo mbili. Vipi basi mtu ataweza kusema kwamba Hadiyth Swahiyh zimezuliwa kwa sababu ya kufikiria huku? Lau mlango huu ungefunguliwa, basi Hadiyth nyingi Swahiyh zingelihukumiwa kuwa ni batili, kitu ambacho Allaah wala waumini hawakikubali.

[1] Sa´d bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: ”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha milango ya msikitini yote ifungwe isipokuwa tu mlango wa ´Aliy.” (Ahmad 1/175).

[2] Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: ”Janaabah hutumiwa kwa mambo mawili: kumwaga na jimaa.” (Fath Dhil-Jalaal wal-Ikraam (1/573)).

  • Mhusika: Haafidhw Ahmad bin ´Aliy bin Hajar al-´Asqalaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qawl al-Musaddad, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 08/12/2018