Fungua mgahawa jioni Ramadhaan na mchana funga!


Swali: Je, inafaa kwa muislamu kufungua mgahawa katika nchi isiyokuwa ya waislamu mchana wa Ramadhaan kuwafungulia makafiri?

Jibu: Ndugu mpenzi muislamu! Wewe umefunga. Mchana kwako ni wenye kuheshimiwa. Makafiri hawa hawauheshimu. Wanaukiuka. Kwa sababu wao kimsingi si wenye kuwalazimu katika wakati kama huu. Ni makafiri. Masuala ya kwamba mataga ya Shari´ah ni yenye kuwagusa tumekwishawazungumzieni na hatutaki mturudishe tena huko. Usiwasaidie kukiuka heshima ya michana hii ilihali wewe ni muislamu. Fungua badala yake mida ya jioni.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Gi8-wIY2jn4
  • Imechapishwa: 22/05/2018