Funga simu unapokuja msikitini


Swali: Wako watu wengi ambao wanatumia simu zao misikitini wakati wa mihadhara ya kidini na darsa za kielimu. Je, kitendo hichi kweli kinastahiki? Ni kipi cha wajibu kwetu juu ya watu hawa kwa sababu wanawashawishi waswaliji na wale waliohudhuria? Ni ipi hukumu ya nyimbo zinazopatikana katika simu hizi?

Jibu: Inatakikana kwa yule aliye na simu aizime pale atapoingia msikitini au kuketi kwa ajili ya kusoma ili asije kuwashawishi ndugu zake na asiwaudhi. Simu pia ikiwa na sauti ya muziki haifai. Ama simu iliwa na sauti ya kawaida basi aizime mpaak atapomaliza kuswali na akatoka msikitini. Ama kuiacha wazi wakati wa swalah au wakati wa darsa, jambo hili ndani yake kuna ushawishi. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba imechukizwa. Kuna misikiti imeandikwa baadhi ya ilani zinazowataka watu kuzima simu zao. Lakini watu wengi wanachukulia sahali na wako wengine wanaosahau. Mtu anatakiwa kulipupia jambo hili mpaka asiweze kusahau. Mtu ajaribu kuzima simu yake mpaka atoke msikitini. Lengo asiwashawishi na kuwaudhi ndugu zake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 01/07/2018