Swali: Nina msichana aliye na kitu katika wasiwasi katika wudhuu´ na swalah. Kila anaponiuliza kuhusiana na hilo namwambia kuwa halimdhuru, na kwamba ayapuuze na swalah yake ni sahihi. Je, kitendo changu ni sahihi au kina kufanya wepesi na uzembeaji?

Jibu: Hapana, ni sahihi. Ukiongezea juu ya hilo atake kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa. Kwa sababu akijifungulia kwenye nafsi yake mlango wa wasiwasi yatamzidi. Aufunge kwa kutaka ulinzi dhidi ya shaytwaan na kuachana na wasiwasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%204%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017