Swali: Naswali swalah za usiku, nafunga mchana na nasoma Qur-aan. Lakini pamoja na haya yote bado ni mwenye kuendelea kujitoa manii na sijaweza kujikwamua na jambo hilo. Kuna njia ipi ya Kishari´ah ya kujinasua na hilo?

Jibu: Ina maana kwamba una matamanio mengi. Ni wajibu kwako kufunga. Funga kwa wingi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameelekeza katika swawm:

“… yule asiyeweza kuoa basi afunge. Kwani hiyo kwake ni kinga.”

Funga kwa wingi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-1-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 18/02/2018