Fiqh kuhusu kumpa mtoto mchanga jina


Swali: Hukumu ya kuwapa watoto majina haya “al-Juuriy”, “ad-Daanah”, “Ghaayah” na “Ghaaliyah”?

Jibu: Ndio, hakuna ubaya. Kila jina lisilokuwa na uabudiwa badaya Allaah hakuna neno. Haramu ni yale yenye uabudiwa badala ya Allaah. Kama ´Abdul-Husayn, ´Abdur-Rasuul au ´Abd (mja wa) wa fulani au amiri. Haya ni haramu haijuzu. Kuelekeza uiabudiwa kwa asiyekuwa Allaah haijuzu kwa Ijmaa´. Ama majini yasiyokuwa na uabudiwa badala ya Allaah hakuna makatazo. Lakini bora ni kuchagua majina mazuri, hili ni bora. Hakuna ubaya kwa majina haya hata kama bora zaidi kwake angelichagua bora kuliko hayo. Na kule familia kuitwa kwa majina yao wababa, wababu zao na wamama zao, hili ni bora kwa ajili ya malezi.

Swali: Familia yake inaitwa Majiyd. Je, ni lazima walibadili?

Jibu: Hakuna neno ikaitwa Majiyd hata kama katika Majina ya Allaah moja wapo ni Majiyd. Hakuna neno kuitwa kwa jina hata kama ni katika Majina ya Allaah; kama ´Aziyz na Maalik. Ni jambo lajulikana kuwa Majina na Sifa za Allaah si kama ya viumbe. Havifanani hata kama vitafanana kwa matamshi, havifanani kwa uhakika wake na maana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=QI5if_oUYCs
  • Imechapishwa: 11/01/2018