Fikira mbaya za Suufiyyaj juu ya ´ibaadah

Swali: Baadhi ya Suufiyyah wanaona kuwa mja anaweza kufikia katika ngazi ambayo anamwabudu Allaah pasi na kuwa na woga juu ya adhabu Yake wala matarajio juu ya thawabu Zake, isipokuwa anamwabudu Allaah tu ili amshukuru…

Jibu: Huu ni upotevu. Huu ni upotevu na ni kutoka nje ya Qur-aan na Sunnah. Wanasema kwamba hawamwabudu Allaah kwa kuogopa adhabu Yake wala kwa matarajio ya thawabu Zake, isipokuwa wanamwabudu Allaah kwa sababu wanampenda. Hii ni njia ya Suufiyyah.

Tunamwabudu Allaah, tunampenda, tunamwogopa na tunamtarajia Yeye.

Swali: Wanatumia hoja kwa Hadiyth inayosema:

“Je, nisiwe mja mwenye kushukuru?”

Jibu: Hii sio dalili yenye kuwasapoti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisimama muda mrefu na kuswali, mpaka miguu yake inavimba. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akamwambia: “Kwa nini wafanya hivo ilihali Allaah amekusamehe dhambi zako zilizotangulia na zitazokuja?”, ndipo akajibu:

“Je, nisiwe mja mwenye kushukuru?”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (79) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-11-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 28/10/2018