Fawziy al-Asharriy anaishi kati ya Raafidhwah na Suufiyyah. Katika maisha yake yote mpaka hii leo watu hawajapatapo kuona wala kusikia ana msimamo mtukufu wa ki-Suuniy ambapo anainusuru Sunnah na kuwavunja watu wa Bid´ah na wapotevu. Yuko namna hiyo kwa sababu yuko pamoja nao dhidi ya Ahl-us-Sunnah au ni mwoga?

Juhudi kubwa tunayoiona kutoka kwake anaiweka tu dhidi ya Ahl-us-Sunnah kwa uongo, ujinga na upotoshaji. Ameandika vitabu vine vikiwa na kichwa cha khabari ”ar-Ru´uud as-Swawaa´iqiyyah”, ”al-Burkaan”, ”al-Qaasimah al-Khafidhwah” na vyote ni uongo mtupu na kumfanyia khiyana Rabiy´ na nduguze katika Ahl-us-Sunnah.

Hatuoni nashati yake isipokuwa kuwa dhidi ya Hadiyth zilizomo katika “as-Swahiyh” ya Muslim kwa mfano Hadiyth kuhusu kufunga siku ya ´Arafah na kuhusu uombezi. Ameandika vitabu viwili juu ya hilo. Anaeneza uvumi juu ya “as-Swahiyh” ya Imaam Muslim na kuituhumu kwamba imejaa Hadiyth nyingi mbovu (شاذ).

Uko wapi wewe ukilinganisha na wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah ambao wanabainisha upotevu wa Raafidhwah ambapo mmoja wao ni Muhammad Maalullah al-Bahrayniy (Rahimahu Allaah) ambaye aliweka juhudi kubwa katika kubainisha upotevu na uchafu wa Raafidhwah.

Uko wapi wewe na Ruduud za Ahl-us-Sunnah kwa Suufiyyah na waabudu makaburi?

Uko wapi wewe na vitabu vinavyoitetea “as-Swahiyh” ya Muslim na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuraddi mashambulizi yake?

Uko wapi wewe na Ruduud walizotwangwa Haddaadiyyah ambao wanawapiga vita Ahl-us-Sunnah kwa kutumia jina la Ahl-us-Sunnah? Ni vipi utawaraddi ilihali wewe ni mmoja katika viongozi na walinzi wao?

Wewe uko wapi na wale Murji-ah wa kikweli ambao unawatumia kwa kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah na kuwasingizia na kuwatupia tuhuma mbaya?

Uko wapi, wewe Khalafiy ambaye unataka kuigeuza jihadi dhidi ya wapotevu, ukilinganisha na wale Khawaarij wa kale na wa sasa?

Woga wasaliti wasiishi!

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 09/10/2016