Swali: Kuna mtu aliulizwa akatoa fatwa asiyokuwa nayo uhakika. Anapata dhambi ijapo atapatia?

Jibu: Haijuzu kutoa fatwa pasi na elimu ijapo atapatia. Ni haramu kwake kuzungumza bila ya elimu:

إِنَّمَا يَأْمُرُكُم بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Hakika si vyengine isipokuwa anakuamrisheni maovu na machafu na mseme juu ya Allaah yale msiyoyajua.”[1]

[1] 02:169

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (20) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-6-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 24/01/2020