Fatwa ya ´Awwaam juu ya dawa ya uchawi

Swali: Wako ambao wanasema kwamba miongoni mwa dawa za uchawi wa limbwata ni mtu kumtaliki mke wake talaka moja kisha hapo uchawi utaondoka kwa idhini ya Allaah. Halafu baada ya hapo amrejee. Je, kitendo hichi kinafaa?

Jibu: Hii ni fatwa ya watu wasiokuwa na elimu. Haijawahi kusemwa na wanachuoni. Si kweli. Kutibu uchawi sio kwa kutoa talaka. Kuagua uchawi kunakuwa kwa dawa zinazokubalika Kishari´ah. Sio kwa kutoa talaka. Talaka sio suluhu. Allaah (Ta´ala) anachukia talaka. Isipokuwa kukiwa kuna haja ya kufanya hivo kama wanandoa wameshindwa kutangamana kwa wema au hawapatani. Ama kusema kwamba amtaliki kwa sababu ya dawa sijui mwanachuoni yeyote aliyesema hivi. Hili ni jambo limetangaa kwa wasiokuwa na elimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 04/01/2019