Fanya mambo yako pasina kumuomba mtu kitu

Ukiweza kujifanyia jambo lako peke yako, lililo bora na lililopendekezwa usimuombe kiumbe yeyote. Tunachomaanisha kwa kusema “ukiweza”, bi maana bila ya kujikalifisha na bila ya uzito. Yule ambaye mazoea yake siku zote ni kuomba vitu, hili ni jambo limechukizwa. Kinachotakikana kwa mtu ni ajizoweze siku zote kufanya mambo yake mengi anayohitajia [pasi na kumuomba msaada yeyote].

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 284
  • Imechapishwa: 14/05/2020