Faida za Salaam


Kueneza salamu ni sababu ya kuingia Peponi ambayo kila mtu anataka kuifikia. Dalili ya hilo ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hamtoingia Peponi mpaka muamini na hamtoamini mpaka mpendane. Je, nikujuzeni kitu ambacho mkikifanya mtapendana? Toleaneni salamu baina yenu.”

Kutoleana salamu ni miongoni mwa sababu za kupendana, kupendana ni katika ukamilifu wa imani na imani inamwingiza mtu Peponi. Kwa hiyo faida zake ni kubwa. Pamoja na kuwa mtu anapata thawabu, watu kushikamana na kupendana, ukiongezea juu ya hayo: ni sababu inayowafanya watu kuingia Peponi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (13)
  • Imechapishwa: 13/08/2017