Swali: Mtu mwema anapomlea mtoto wake katika kusimamisha Sunnah na dini tokea utotoni mwake anapata mfano wa ujira wake?

Jibu: Ndio, Allaah akitaka. Akimlea na kumkuza juu ya kheri, kisha baba akafariki na mtoto akawa mwema atamuombea baba yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… au mtoto mwema mwenye kumuombea.”

Hawezi kumuombea isipokuwa mpaka awe mwema. Wema una sababu. Nayo ni malezi mazuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (17) http://alfawzan.af.org.sa/node/2110
  • Imechapishwa: 09/07/2020