Faida gani kwa mtu mwenye kuingia katika Uislamu wa Qaadiyaaniyyah?

Kuna kundi katika Waislamu ambao wanajinasibisha na Uislamu. Wanashuhudia kwamba hapana mola wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Wanaswali, wanahiji, wanatoa Zakaah na wanafunga. Lakini hata hivyo wanaamini ´Aqiydah batili inayokwenda kinyume na Shari´ah ya Kiislamu katika mambo mengi ya ´Aqiydah ambayo yanajulikana na watu wote. Kati ya Waislamu wanajulikana kwa jina “Qaadiyaaniyyah”, wakati wao wenyewe wanajiita “Ahmadiyyah”. Wana ´Aqiydah potevu inayokwenda kinyume na Uislamu. Katika hayo wanaamini kwamba mlango wa utume baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado unaendelea na utaendelea mpaka siku ya Qiyaamah. Wanaamini mmoja wao amekuja. Ni mtu wanayemfuata na wamejiacha wakadanganywa na wamejisababishia wao wenyewe kuanguka mbali kabisa na Uislamu. Anajulikana kwa jina Mirzaa Ghulaam Ahmad al-Qaadiyaaniy.

Watu hawa wanalingania katika nchi za Ulaya na nyinginezo na kwa masikitiko kwa juhudi kubwa. Wamefanikiwa kuingiza wengi katika watu wa Ulaya kwenye toleo lao la Uislamu. Wanaamini hayo wanayoamini. Katika hayo wanaamini kwamba kuna uwezekano wa kuja Manabii wengine baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), miongoni mwao ni Mirzaa Ghulaam Ahmad. Je, watu hawa ambao wamesilimu kwa Uislamu wa Qaadiyaaniyyah wanasikia kunazungumziwa juu ya uhakika wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na uhakika wa Da´wah yake? Je, utawafaa kitu Uislamu huu au hapana? Jibu lipo katika Hadiyth iliyotangulia:

“Hakuna yeyote katika Ummah huu, myahudi au mnaswara atakayesikia kuhusu mimi na kisha asiniamini, isipokuwa ataingia Motoni.”

Mwenye kusikia kuhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), tabia yake na Shari´ah yake kwa njia isiyokuwa ya uhakika, bado hajamsikia. Katika hali hii mtu huyu hatokuwa miongoni mwa makafiri Motoni kwa kuwa hajasimamiwa na hoja (ukweli), tofauti na wale wanaoamwamini (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kwamba utume baada yake bado unaendelea na I´tiqaad zingine za Qaadiyaaniyyah. Malengo sio kutaja nyingi katika hizo. Lengo la kutaja hii ni kwa kutoa mfano tu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (17)
  • Imechapishwa: 04/09/2020