Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi na [ameumba] jua na mwezi na nyota vimetiishwa kwa amri Yake. Tanabahi! Ni Vyake pekee uumbaji na amri. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

Uumbaji huu mkuu na mkubwa Allaah amewaumba katika siku sita. Yeye ni muweza wa kuwaumba mara moja. Lakini amewaumba kwa muda wa siku sita kwa hekima anayoijua Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala). Siku sita hizi ya kwanza yake ni siku ya jumapili na ya mwisho yake ni siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa ndio uumbaji ulikamilika. Kwa ajili hiyo ndio maana siku hii ikawa ni siku tukufu zaidi ya wiki. Siku hiyo ndio bwana ya masiku, sikukuu ya wiki na ndio siku bora zaidi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema.

“Siku bora iliyochomozewa na jua na siku ya ijumaa.”[2]

Kwa sababu siku hiyo ndio kulikamilika uumbaji wa viumbe. Siku hiyo ndio ameumbwa Aadam, siku hiyo ndio kaingia Peponi na siku hiyo ndio akashuka kutoka ndani yake. Siku ya ijumaa ndio Qiyaamah kitasimama. Yote hayo siku ya ijumaa. Ndio siku bora. Ndio siku ya mwisho ya uumbaji wa mbingu, ardhi na vilivyomo ndani yavyo.

[1] 07:54

[2] Muslim (854), Abu Daawuud (1046), at-Tirmidhiy (488) na an-Nasaa´iy (03/90).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-uth-Thalaathah, uk. 111-113
  • Imechapishwa: 14/02/2020