Fadhila za maji ya zamzam ni Makkah peke yake?


Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maji ya zamzam ni kwa kile alichonuia mtu.”

Je, hili ni pale tu ambapo mtu atayanywa akiwa Makkah?

Jibu: Hapana. Inafaa kuyatoa sehemu moja hadi nyingine, kuyatumia na kujitibu kwayo sehemu yoyote. Kwa sababu fadhila zake zimeambatana nayo na bado zimebaki. Inahusu sehemu yoyote pale.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (66) http://alfawzan.af.org.sa/node/16524
  • Imechapishwa: 13/08/2017