Endelea kutahadharisha nao


Swali: Nimeandika makala kwa lengo la kuitetea nchi hii Saudi Arabia iliyobarikiwa na kubainisha khatari ya al-Ikhwaan al-Muslimuun inayopata michango kutoka Qatar. Baadhi ya walinganizi wakasema kuwa ni fitina ambayo haitakiwi kuingiliwa. Wanamtuhumu yule mwenye kuitetea nchi hii ya kwamba ni Jaamiy. Ni yepi maoni yako juu ya hilo?

Jibu: Waulize Jaamiy ni kitu gani.

Muulizaji: Wanasema kuwa Jaamiy ni mtu anayehimiza katika usikizi na utiifu.

Jibu: Mtu kama huyo ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Sio Jaamiy. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ndio wanaoamrisha usikizi na utiifu.

Swali: Unawashauri vipi wale wanaosema kuwa kuwatahadharisha al-Ikhwaan al-Muslimuun ni fitina isiyotakiwa kuingiliwa?

Jibu: Achana nao. Endelea na achana nao.

Swali: Tuendelee?

Jibu: Ndio.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=FnQry2kpHeU&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 06/08/2017