Swali: Hadiyth isemayo:

“Anapofariki mwanaadamu basi matendo yake yote yanakatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika kwayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”[1]

Je, elimu za kudunia pia zinaingia katika Hadiyth hii kama elimu ya hesabu na matibabu?

Jibu: Hapana. Haidyth inakusudia elimu ya Kishari´ah na sio elimu za kidunia. Bila shaka zimeruhusiwa, lakini hazichukui hukumu ya Kishari´ah.

[1] Muslim (1631).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (49) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/m-3%20%20-%2012%20-%202%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/10/2018