“Ee Allaah! Sikuombi kurudi nyuma kwa Qadar lakini nakuomba upole ndani yake”

Swali: Nimesikia kutoka kwa baadhi kwamba haijuzu kuomba du´aa kwa kusema:

اللهم لا أسألك رد القضاء بل أسألك اللطف فيه

“Ee Allaah! Sikuombi kurudi nyuma kwa Qadar lakini nakuomba upole ndani yake.”

Jibu: Hapana, hayasihi maneno haya. Mtu asisemi hivi. Badala yake mtu aseme:

اللهم اعف عني، اللهم اغفر لي، اللهم ارحمني، اللهم أجرني من النار، اللهم إني أعوذ بك من الشر كله

“Ee Allaah nisamehe, nighufurie, nirehemu, niepushe na moto na nilinde kutokamanaad na shari zote.”

Kila kitu kinatokana na Qadar. Du´aa inaingia ndani ya Qadar. Mtu anatakiwa amwombe Allaah amuepushe kutokamana na shari zote, amtunuku msimamo katika dini, uongofu, kutengemaa, amkunjulie riziki yake, amsaidie dhidi ya shaytwaan, manaibu wake na wasaidizi wake. Kwa msemo mwingine amwombe Mola wake kheri na ajilinde Kwake kutokamana na shari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3034/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%82%D9%88%D9%84-%D9%84%D8%A7-%D8%A7%D8%B3%D8%A7%D9%84%D9%83-%D8%B1%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%B6%D8%A7%D8%A1-%D8%A8%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%84%D8%B7%D9%81
  • Imechapishwa: 13/02/2020