Duyyuuth ni nani kwa mtazamo wa Kiislamu?


Swali: Je, Duyyuuth ni yule ambaye anaelezea yanayopitika baina yake yeye na mke wake kitandani au ni nani Duyyuuth kwa mtazamo sahihi wa Kiislamu?

Jibu: Duyyuuth ni yule ambaye anaridhia machafu ya mke wake, anaridhia kuchukuliwa mke wake, anaridhia mke wake kufanywa Zinaa. Huyu ndiye Duyyuuth. Ni yule ambaye anaridhia kuchukuliwa mke wake na kutumiwa, pasina kuwa na wivu wala kujali. Kwa kuwa na na Imani pungufu au kutokuwa nayo kabisa. Huyu ndiye huitwa Duyyuuth. Ama yule ambaye anaelezea hali yake na mke wake, haya ni maasi na anaweza kuwa fasiki kwa hilo. Lakini hawi Duyyuuth. Duyyuuth ni yule ambaye anaridhia machafu ya mke wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 31/03/2018