al-Haafidhw al-Mizziy amesema:

“al-Husayn bin Waaqid na wengineo wameeleza kwamba Anas amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliniombea du´aa akasema:

اللهم أكثر ماله و ولده، و أطل حياته

”Ee Allaah!  Mkithirishie mali na kizazi chake na urefushe uhai wake.”[1]

Inafahamisha kwamba inafaa kumwombea mtu du´aa ya maisha marefu, kama ilivyozoeleka katika baadhi ya miji ya kiarabu, tofauti na wanavosema baadhi ya wanachuoni. Linalotilia nguvu hilo ni kwamba hakuna tofauti kati ya du´aa hii na du´aa ya kufuzu na mengineyo, kwa sababu yote hayo ni yenye kukadiriwa.

[1] Tahdhiyb-ul-Kamaal (2/364).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (5/288)
  • Imechapishwa: 24/07/2020