Du´aa ya Istikhaarah inaombwa baada ya kumaliza kuswali

Swali: Ni lini kunasomwa du´aa ya Istikhaarah; nje ya swalah nikikusudia baada ya kumaliza kuswali au katikati ya swalah? Je, kuna tofauti kati ya kusoma du´aa ya Istikhaarah kutoka katika kitabu au karatasi au kuisoma kwa hifdhi? Je, imesuniwa kuirudi swalah ya Istikhaarah mara nyingi juu ya kitu hichohicho?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah kwa muislamu akiswali swalah ya Istikhaarah basi aombe du´aa baada ya kumaliza kuswali. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu akikusudia kufanya jambo, basi aswali Rak´ah mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ

”Ee Allaah! Hakika mimi nakutaka ushauri kwa ujuzi Wako… “

Hii ni dalili inayojulisha kwamba du´aa inakuwa baada ya kutoa salamu ya swalah. Bora ni yeye anyanyue mikono yake. Kwa sababu kunyanyua kwake mikono ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa du´aa. Hadiyth ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh). Andiko lake ni kama ifuatavyo: ”Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwa kusema:

”Mtume wa Allaah  alikuwa akitufundisha Istikhaarah katika mambo yote kama vile anavyotufunza Suurah ndani ya Qur-aan. Akisema: ”Mmoja wenu akikusudia kufanya jambo, basi aswali Rak´ah mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ، وَأَسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ، وَأَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ العَظِيمِ، فَإِنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أَقْدِرُ، وَتَعْلَمُ وَلاَ أَعْلَمُ، وَأَنْتَ عَلَّامُ الغُيُوبِ، اللَّهُمَّ إِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ خَيْرٌ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي – أَوْ قَالَ: عَاجِلِ أَمْرِي وَآجِلِهِ – فَاقْدُرْهُ لِي، وَيَسِّرْهُ لِي، ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ، وَإِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ شَرٌّ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي – أَوْ قَالَ عَاجِلِ وَآجِلِهِ – فَاصْرِفْهُ عَنِّي، وَاصْرِفْنِي عَنْهُ، وَاقْدُرْ لِي الخَيْرَ حَيْثُ كَانَ، ثُمَّ أَرْضِنِي به

”Ee Allaah! Hakika mimi nakutaka ushauri kwa ujuzi Wako na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako na nakuomba kutokana na fadhilah Zako tukufu. Hakika Wewe unaweza, nami siwezi, unajua, nami sijui Nawe ni mjuzi wa yaliyofichikana. Ee Allaah! Iwapo unajua kuwa jambo hili lina kheri nami katika dini yangu, maisha yangu na mwisho wa jambo langu” – au alisema: ”Duniani na Aakhirah” – basi nakuomba uniwezeshe nilipate na unifanyie wepesi kisha unibarikie kwacho. Endapo unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu, maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liweke mbali nami, uniepushe nalo na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, halafu niridhishe kwalo.”[1]

Imetolewa na al-Bukhaariy.

[1] al-Bukhaariy (1096).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/422)
  • Imechapishwa: 17/11/2021