Swali: Ni ipi hukumu ya kunyunyua mikono katika du´aa ya Khutbah ya Ijumaa?

Jibu: Haijuzu, kwa imamu na maamu, kunyanyua mikono katika du´aa ya siku ya Ijumaa. Isipokuwa katika du´aa ya kuomba kunyweshelezewa. Akimuomba mvua katika du´aa ya siku ya Ijumaa wanyanyue mikono yao. Mbali na du´aa ya kunyweshelezewa siku ya Ijumaa kusinyanyuliwe mikono.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13980
  • Imechapishwa: 11/04/2018