Du´aa ni miongoni mwa sababu kubwa

Swali: Tumesoma kwamba tumeamrishwa kufanya sababu. Wanachuoni wamesema kwamba kuomba du´aa ni miongoni mwa sababu kubwa. Je, inawezekana kutendea kazi sababu hii pekee na mtu akatosheka kwayo?

Jibu: Hapana, usitosheke kwayo. Fanya sababu zengine zilizoruhusiwa zaidi ya kuomba du´aa tu. Kuomba du´aa ni moja katika sababu. Ikiwa unataka kufa kwa sababu ya njaa utasema kuwa huli na inatosha tu kuomba du´aa? Hapana. Ni lazima ufanye sababu zengine za kilazima pamoja na kuomba du´aa. Ikiwa umepatwa na maradhi makali na dawa ipo utaacha kujitibisha kwa madai eti unatosheka tu kuomba du´aa? Hapana, si sawa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (14) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-03-11-1434.mp3
  • Imechapishwa: 14/06/2019