Du´aa ni aina kubwa ya ´ibaadah

Swali: Mtunzi wa kitabu anakusudia nini anaposema kwamba:

“Du´aa ndio ´ibaadah.”?

Kwani du´aa ndio msingi wa Tawhiyd?

Jibu:

“Du´aa ndio ´ibaadah.”

Du´aa ndio ´ibaadah yenyewe. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ

 “Niombeni Nitakuitikieni.”[1]

Kisha akasema:

إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ

”Hakika wale wanaotakabari na kuniabudu wataingia Jahanam wadhalilike.”[2]

Hivyo (Subhaanahu wa Ta´ala) akaiita kuwa ni ´ibaadah.

[1] 40:60

[2] 40:60

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 59
  • Imechapishwa: 04/07/2019