Swali: Mtu akimuombea du´aa mbaya ambaye amemdhulumu au ambaye anadhihirisha waziwazi baadhi ya madhambi makubwa kwamba Allaah awaangamize watoto wake au awafanye kuwa wagonjwa – je, du´aa mfano wa hii inakubaliwa ingawa wao hawakumshambulia wala hawakumdhulumu?

Jibu: Haifai kwake kufanya hivo. Haitakikani kwa mtu kuomba dhidi yake. Bali anatakiwa kumuombea uongofu. Ambaye kamdhulumu anapaswa kumsamehe. Akimsamehe ndio bora. Amesema (Ta´ala):

وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ

“Mkisamehe ni ukaribu zaidi wa kumcha Allaah.”[1]

فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ

”Atakayesamehe na akatengeneza, basi ujira wake uko kwa Allaah.”[2]

Pengine wakati wa kuomba dhidi ya aliyemdhulumu akaongeza katika du´aa yake. Yule mwenye kuombewa dhidi yake akachukua ziada kutoka kwake [siku ya Qiyaamah].

[1] 02:237

[2] 4240

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 12/09/2021