Swali: Kuna du´aa iliyosuniwa mtu kusema ili apate kusalimika kutokamana na kujionyesha (الرياء)?

Jibu: Kuna du´aa inayotambulika:

اللهم إني أعوذُ بك أن أشرِكَ بك و أنا أعلمُ ، و أستغفِرُك لما لا أَعلمُ

“Ee Allaah! Najilinda Kwako kukushirikisha Wewe ilihali najua na Unisamehe kwa yale nisiyoyajua.“[1]

Du´aa hii inaombwa siku zote. Inatakikana kwa muislamu daima aombe du´aa hii.

Swali: Aombe du´aa hii kabla ya kuanza kitendo chochote?

Jibu: Nyakati zote.

[1] Ahmad (1906). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh al-Adab al-Mufrad” (551).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21904/ما-الدعاء-المشروع-لمن-خشي-الرياء
  • Imechapishwa: 29/09/2022