Swali: Kuna du´aa dhidi ya wasiwasi?

Jibu: Ndio. Atake kinga dhidi ya shaytwaan. Wasiwasi unatokamana na shaytwaan. Akihisi wasiwasi atake kinga dhidi ya shaytwaan:

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

“Utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi.” (41:36)

Anachotakiwa ni yeye kumuomba Allaah kinga dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa na apuuzie wasiwasi. Kwa idhini ya Allaah utamwondoka. Asiujali, si katika swalah, wudhuu´ wala kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%204%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017