Dogo Liwezalo Kusemwa Kwa Mtu Mwenye Kutangamana Na Ahl-ul-Bid´ah


Swali: Ni ipi hukumu ya kutangamana na Hizbiyuun, au na watu ambao wanajulikana kwa Hizbiyyah kwa hoja ya kuwa anajua yalio kwa watu hawa?

Jibu: Ni jambo la ajabu, geni na hoja dhaifu sana. Nadhani kila mtu mwenye akili hujitenga kutembea pamoja na fasiki na watu wachafu ambaowatu wanawajua kwa maovu. Unasikia haya watu kukuona pamoja nao. Kwa nini? Ili watu wasidhani kuwa wewe ni kama yeye. Hali ikiwa ni namna hii kwa mtu fasiki, tusemeje kwa mzushi?

Kwa hivyo, nasema kuwa kutangamana na Hizbiy na mzushi haijuzu. Kwa nini? Kwa kuwa ukitembea nae, hata kama utakuwa ni katika Ahl-us-Sunnah, dogo liwezalo kusemwa kwa mtu asiyejua atakuchukulia wewe ni kama yeye. Akikuona unatembea nae atakhitimisha kwa kusema kuwa huyu ni rafiki ya fulani. Hili ni katika mazuri na mabaya. Wakimuona mtu anatembea na mwanachuoni, watasema kuwa huyu ni mwanafunzi wa mwanachuoni huyu. Baada ya hapo watakhitimisha kuwa anamtakasa. Ni kweli ama si kweli? Na kinyume chake. Na anapokuja mpotevu watasema kuwa huyu ni rafiki wa fulani. Baada ya hapo watakhitimisha na kuanza kumponda na kumjeruhi.

Hivyo, wewe ukitembea na watu hawa, bila kujali sababu yoyote, watu watakuchukulia wewe ni kama wao. Kwa ajili hii tokea zamani kulikuwa kunasemwa:

Usimuulizie mtu fulani – mtazame rafiki yake. Kila rafiki huiga kama alivyo mwenzake.

Hawezi kutembea nae isipokuwa naye atakuwa katika madhehebu yake. Hapo ndipo ambapo utakuwa wewe mwenyewe unajichangia shubuha na dhana mbaya na wakati ambapo wewe hufuati madhehebu yao. Hii inatosha kuwa sababu kwako kujitenga mbali na Ahl-ul-Ahwaa´. Vipi kusemweje kwa sababu ya kutembea kwako nao lau utatumbukia katika Bid´ah za mtu huyo?

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=38255
  • Imechapishwa: 09/11/2014