Swali: Mimi ni mtu ambaye nina watoto. Nilikuwa na dishi ambapo Allaah akaniongoza na nikaiacha. Je, inajuzu kwangu kumuuzia mtu mwengine?

Jibu: Ukimuuzia dishi mtu mwengine ataifanya nyinyi? Ataitumia katika mambo ya haramu. Wewe utakuwa umemsaidia katika mambo ya haramu. Tuchukulie muulizaji anasema kwamba anataka kumpa zawadi mtu na huku anatafuta Uso wa Allaah. Inajuzu? Haijuzu kufanya hivi. Si sawa kuutafuta Uso na radhi za Allaah kwa kitu cha haramu. Haifai kujikurubisha kwa Allaah isipokuwa kwa matendo mema. Kwa hivyo si halali. Haifai hata kumpa kwa bure. Nifanye nini sasa? Ivunje[1]. Akiivunja kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) basi Allaah atampa badala yake kilicho bora kuliko hiyo…

Kwa hivyo tunamwambia ndugu huyu ambaye Allaah amemwongoza na akaacha kusikiliza na kutazama dishi aivunje. Nakupa bishara kwamba Allaah atakupa badala yake kitu bora.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/televisheni-yangu-niifanye-nini/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/784
  • Imechapishwa: 20/01/2018