Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Mwisho mwema ni wa wamchao na muovu ni kwa madhalimu. Swalah na salaam zimwendee yule ambaye Allaah amemtuma akiwa ni huruma kwa walimwengu; Mtume wetu Muhammad swalah na salaam zimwendee yeye na kizazi chake.

Amma ba´d:

Hii ni chapa ya kumi ya kitabu “al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd”.

Ninakitoa kichapishwe baada ya kuipitia chapa iliyotangulia. Chapa hii ina makaguzi yenye faida. Ninamuomba Allaah mkarimu na mtukufu kwa majina na sifa Zake ajaalie kiwe kimefanywa kwa ajili Yake Pekee na awanufaishe kwacho waislamu, kuanzia masharini mpaka magharibi – hakika Mola Wangu ni mwenye kusikia du´aa. Nimekipangilia, kufuta na kuongeza vitu pale panapostahiki kufanya hivo. Ninamuomba Allaah anijaalie mimi na ndugu zangu waumini elimu yenye manufaa na matendo mema, kufuzu kwa kuipata Pepo na kusalimika na
Moto.

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad na kizazi chake.

Msikiti wa as-Sunnah, Hudaydah

15 Ramadhaan 1429

Abu Ibraahiym Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy al-´Abdaliy§

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd
  • Imechapishwa: 05/08/2020