Swali: Kuna wanaosema wale wenye kusema Dhikr kwa sauti baada ya Swalah ya kwamba wanapata dhambi. Ni upi usahihi wa maneno yao haya?

Jibu: Huyu ndiye mwenye dhambi kwa kuwa anapinga Sunnah. Kusema Adhkaar kwa sauti baada ya Swalah ndio Sunnah iliyothibiti kwa Maswahabah pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aliwakubalia hilo (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). Mwenye kusema kuwa wanapata dhambi yeye ndiye mwenye kupata dhambi kwa kupinga kwake Sunnah.

Ni wajibu kwa mtu ihifadhi ulimi wake kwa kuzungumza asiyoyajua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_13.mp3
  • Imechapishwa: 19/06/2018