Swali: Dhambi kubwa zinamtoa mtu katika Uislamu?

Jibu: Dhambi kubwa ikiwa ni shirki au kufuru zinamtoa mtu katika Uislamu. Ama ikiwa siyo hayo hayamtoi mtu nje ya Uislamu. Lakini zinaipunguza imani na kumfanya mtu akawa ni mwenye imani pungufu. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.” (an-Nisaa´ 04:48)

Dhambi kubwa ambazo ni chini ya shirki hazimtoi mtu katika Uislamu. Lakini mwenye nayo anahukumiwa kuwa ni muumini mwenye imani pungufu na anahukumiwa vilevile kutenda dhambi nzito (Fisq). Yuko chini ya utashi wa Allaah; akitaka atamsamehe na asipotaka atamuadhibu. Lakini hata hivyo hatodumishwa Motoni milele. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (04) https://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/04.mp3
  • Imechapishwa: 27/11/2019