Swali: Vipi kuelezea Da´wah hii ya Kiislamu ya kwamba ni ”Wahhaabiyyah”. Ni yapi maelekezo yako juu ya maneno na hujuma kama hizi?

Jibu: Da´wah inanasibishwa kwa mwenye nayo ikiwa yeye ndiye kaizua. Ikiwa yale aliyolingania mtu huyo ni yenye kuafikiana na Qur-aan na Sunnah basi hainasibishwi kwake. Bali ni Da´wah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sio Da´wah ya Wahhaabiyyah. Hakuna ilichofanya Da´wah ya Wahhaabiyyah isipokuwa tu imekuja kuhuisha na kuwawekea watu wazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17206
  • Imechapishwa: 30/12/2017