Da´wah Salafiyyah itaendelea kusonga mbele na haitodhurika na vitimbi vya wapuuzi na wanafiki

Swali: Tunaomba uwape nasaha waislamu wengi ndani ya nchi na nje ya nchi ambao imekuwa kazi yao ni kuleta utata juu ya Da´wah hii na wanadai, kutokamana na ujinga, ya kwamba kushikamana nayo kunapelekea kuleta vurugu kwa waislamu katika nchi hii na nyenginezo.

Jibu: Hapana shaka ya kwamba Da´wah hii ina maadui na wapinzani tokea hapo kale wakati wa Shaykh. Lakini kwa vile ni Da´wah ya kweli na yenye kutengeneza haikudhurika na hayo. Iliendelea kushika njia yake na haikudhurika na hayo na haikusita kwa kupatikana wapinzani na wapuuzi. Hili ni jambo lililokuwepo tokea hapo kale. Walikuwepo wapuuzi, wanafiki na maadui tokea hapo kale. Lakini hatuwajali na mambo yao hayatushughulishi. Tunaendelea na njia yetu. Hatuwajali wale wenye kuikosesha nusura na wale wenye kuipa majina bandia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17206
  • Imechapishwa: 01/01/2018