Swali: Walinganizi wamekuwa wengi leo lakini hata hivyo ni wachache katika wao wanaolingania katika Tawhiyd na ´Aqiydah. Je, asiyelingania katika Tawhiyd anazingatiwa kuwa anaenda kinyume na Mitume na hivyo kutahadharishwe juu ya Da´wah yake?

Jibu: Ndio, kutahadharishwe. Asiyelingania katika Tawhiyd na anasema kuwa Tawhiyd sio lazima. Badala yake kutahadharishwe madhambi, maasi, ribaa, zinaa na mfano wa hayo, hii ni Da´wah isiyokuwa na kichwa. Ni kama mfano wa mwili usiokuwa na kichwa. Kuna mwili usiokuwa na kichwa ukawa hai? Hapana. Ni maiti. Hii ni Da´wah maiti ambayo hakuna faida nyuma yake. Da´wah hii inaenda kinyume na Da´wah ya Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam). Kitu cha kwanza walichokuwa wakianza nacho ni Tawhiyd. Tawhiyd ikithibiti na kuhakikishwa ndio sasa wanawafunza watu mambo ya dini yao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh):

“Iwe kitu cha kwanza utacholingania kwacho “Kuhushudia ya kwamba mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Wakikuitikia katika hilo wafunze kuwa Allaah amewafaradhishia swalah tano mchana na usiku… “

Wasipomuitikia Tawhiyd hakuna faida ya hayo mengine. Lau wataswali usiku na mchana swalah zao hazina faida yoyote.

Kila Da´wah isiyotilia umuhimu Tawhiyd basi hiyo ni Da´wah maiti na haizalishi kitu kamwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (16) http://alfawzan.af.org.sa/node/2109
  • Imechapishwa: 05/07/2020