Da´wah haihitajii picha


Ninaapa kwa Allaah ya kwamba sijuzishi picha. Sizipendi na wala siko radhi nazo. Yule atakayesambaza picha yangu basi mimi nitakuwa mtesi wake siku ya Qiyaamah. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba siko radhi zao.  Ni vipi nitakuwa radhi nazo ilihali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha? Amemlaani mtu mwenye kula riba, mwenye kuitoa, wale mashahidi wawili wenye kuishuhudia na mpiga picha. Haya yamepokelewa katika “as-Swahiyh” ya Muslim. Enyi watu! Tuzifanye nini dalili zote hizi?

Wanachuoni wote wameziruhusu wakati wa dharurah, lakini picha hizi sio dharurah.  Tuzifanye nini dalili zote hizi? Hii sio dharurah. Kitabu cha Allaah kimefikishwa kwetu kutoka kwa mtu hadi kwa mtu, Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zimefikishwa kwetu kwa milolongo ya wapokezi na kutoka kwa mtu hadi mtu. Lau mapicha haya yangelikuwa ni sharti basi picha za watu hawa zingefikishwa kwetu na zikahifadhiwa. Katika hali hii wao wangelikuwa na haki zaidi ya kufanya hivo. Nukuu sahihi zinatosha. Hii leo tuko mpaka na sauti. Unamsikia mwenye kuzungumza kana kwamba yuko mbele yako. Haya yanatosha na himdi zote ni za Allaah.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://a.top4top.net/m_562c0vm61.mp3
  • Imechapishwa: 29/07/2017