Dawa ya wasiwasi baada ya kukidhi haja

Swali: Je, imepokelewa kutoka kwa Imaam Ahmad ya kwamba mtu akiwa na wasiwasi juu ya kuvuja kitu basi aoshe na maji kwenye chupi yake baada ya kukidhi haja?

Jibu: Sijui kama Imaam Ahmad amesema hivo, lakini wanasema hivo. Lakini baadhi ya wanachuoni waliokutana wamesema hivo. Wanasema ikiwa mtu yuko na wasiwasi kuwa ametokwa na kitu aoshe chupi yake na maji ili wasiwasi umuondokee.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017