Dawa ya mwenye wasiwasi katika ´Ibaadah


Swali: Kuna kijana anasumbuliwa na wasiwasi katika Basmalah, wudhuu´, twahara, wakati wa kujisafisha na maji kwa kukidhi haja na wakati wa kuswali. Ni ipi dawa kwa sababu analeta Takbiyrah katika swalah na huku anajiambia kuwa hajaleta Takbiyrah na anahisi kuwa upepo umemtoka?

Jibu: Apuuze wasiwasi na kuutupilia mbali na kuachana nao, endelee na swalah, ´ibaadah zake na twahara yake. Hana juu yake kitu. Akihisi wasiwasi aombe kinga kwa Allaah dhidi shaytwaan na apuuze haya na huku aendelee na kitendo chake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14005
  • Imechapishwa: 18/04/2018